Habari

Wakati Tanzania ikisubiri ndege yake ya Dreamliner, Ethiopian Airlines waweka rekodi hii barani Afrika

Wakati Watanzania wakisubiri ujio wa ndege kubwa na ya kisasa ya Dreamliner ambayo ndio itakuwa ndege kubwa zaidi kwa shirika la Air Tanzania, shirika la Ethiopian Airline limejiwekea rekodi barani Afrika kwa kuagiza toleo jipya la Being 787 Max 8 ambalo limetoka mwaka 2013.

Shirika la ndege la Ethiopia limepokea ndege hiyo leo asubuhi jijini Addis Ababa na inakuwa ndiyo ndege ya kwanza kumilikiwa na shirika la ndege kutoka Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Kampuni ya Boeing, Tewolde GebreMariam amesema kuwa kukua kwa biashara ya usafirishaji wa anga barani Afrika kumepelekea makampuni mengi kuimarika kiuchumi.

Kwa mujibu wa maelezo ya mtandao wa Kampuni ya Boeing, Ethiopian Airline wana order ya ndege kama hizo 30 na gharama ya ndege moja ni dola milioni $110 sawa na tsh bilioni 250 .

Ndege hiyo inauwezo wa kuchukua abiria hadi 215 na kutembea umbali wa kilometa 6,650 angani bila kusimama.

Shirika la Ethiopian Airline linatajwa kuwa moja ya mashirika bora zaidi ya ndege barani Afrika na linakadiriwa kuwa na ndege kubwa zaidi ya 90.

Hata hivyo, licha ya kuwa ndege hiyo ni toleo jipya la Boeing lakini bado inakuwa ndogo ukilinganisha na matoleo ya Dreamliner kama Dreamliner 787-8 iliyoagizwa na Tanzania.

Ndege iliyoagizwa na Tanzania, Dreamliner 787-8 yenye uwezo wa kuchukua abiria zaidi ya 250.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents