Burudani

Wakazi amshangaa Malaika, ‘hata Diamond, Alikiba hajawafikia’… kisa?

Baada ya msanii Malaika kudai yeye ndiye msanii aliyefanya show nyingi zaidi Marekani kutoka Bongo, Rapper Wakazi amesema hilo halina ukweli wowote kwani yeye toka mwaka 2009 anafanya show katika nchi hiyo.

Wakazi ameeleza kuwa muimbaji huyo hawezi kuwa amemfikia kwani yeye amefanya show nyingi zisizo na idadi hadi Marekani ikafika kipindi akaweza kuendesha maisha yake kupitia show pekee.

“Hawezi kuwa amenifikia kufanya show kwa kule kwa sababu nakumbuka mimi mwaka 2009 ndio nilianza kutoa free style za kwanza kwanza, 2010 nikatoa mixtape ya kwanza nikaanza kuwa maarufu kule. Hizo show ambazo anazifanya mimi ndio nakawa booked na kila mwaka nikawa booked, nikawa sikai ikibidi niache kazi ili niwe nafanya show tu, kuna kipindi ilifikia hivyo, so hawezi kuwa amefikia level yangu,” ameiambia The Playlist ya Times Fm na kuongeza.

“Nadhani hata Diamond, Kiba sidhani hata wao amewafikia kwa sababu hata wao wamefanya show nyingi sana ila mimi nimefanya show nyingi sana akija Fid Q Marekani show yake nitakuwepo, akija Professor Jay nitakuwepo, Chameleon show yake nitakuwepo na Mr Nice,” amesema Wakazi.

Wakazi kwa sasa anafanya vizuri na ngoma zake mbili ‘Hapa Wakazi Tu, Bakora’ na ngoma aliyoshirikishwa na Grace Matata ‘Dakika Moja’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents