Habari

Mke wa Kenyatta na Kagame kukutana katika mbio Rwanda

By  | 

Wake wa marais wawili katika jumuia ya Afrika Mashariki, Margaret Kenyatta wa Kenya na Janette Kagame wa Rwanda wanatarajiwa kushiriki katika mbio za kimataifa za amani zitakazofanyika mjini Kigali Jumapili hii.

Mama Kageme na Mama Kenyatta watashiriki mbio za kilomita saba, huku wakiungana na maelfu ya wanariadha wengine 6000 kutoka mataifa mbali mbali na wanadiplomasia watakaoenda masafa ya kilometa 42 na 21. Mbio hizo za Amani zina lengo la kusisitiza amani nchini humo.

Mbio hizo za amani zitafanyika katika uwanja wa Amahoro,uliopo Kigali-Rwanda, ambapo mshindi wa mbio za kilomita 41 ataondoka na dola 2400 za marekani na mshindi wa kilomita 21 akitunukiwa dola 1200 za marekani.

Rais wa shirikisho la riadha nchini Rwanda, Jean Paul Munyandamutsa amesema kuwa mbio hizo zitatanguliwa na shughuli mbalimbali zitakazowashirikisha watoto na vijana siku ya Jumamosi. Mashindano ya mwaka huu yanatarajiwa kuwa na ushindani mkali licha ya wanariadha wa Kenya kushinda kwenye makala ya zamani ya mbio hizo ikiwemo mwaka uliopita.

Na Laila Sued

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments