Habari

Waliorekodi video mtu akizama maji mpaka kufa bila msaada waachiwa huru (+video)

Kundi la vijana watano nchini Marekani walizua gumzo mtandaoni wiki mbili ziliyopita baada ya kuposti video ikiwaonesha wakishangilia na kumrekodi mtu mmoja aliyekuwa anazama kwenye bwawa huku akipiga makelele akiomba msaada wao kumuokoa hatimaye Polisi wa mji wa Cocoa huko Florida wamewaachia huru vijana hao.

Vijana hao wenye umri kati ya miaka 14-19 ambao wanatoka Cocoa, Florida nchini Marekani walimuona mtu huyo aliyetambulika kwa jina la Jamel Dunn (32) akizama lakini hawakumuokoa wala kupiga namba za simu za polisi kutoa taarifa, wameachiwa huru baada ya kuwekwa ndani kwa mahojiano na ushahidi wa video waliyorekodi.

“Video inaonesha walikuwa wanamrekodi na kucheka muda wote huku wakitukana wakati mwenzao akiomba kuokolewa lakini hakuna sheria iliyovunjwa kutokana na katiba yetu tumewaachia huru ingawaje kibinadamu ni kitendo kibaya ambacho hatuna budi kukikemea”,imesomeka ripoti iliyotolewa na Mwanasheria wa mahakama ya Brevard.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka Polisi wa Kituo cha Cocoa ambako vijana hao wanaishi mtaa huo wanasema wakati wakimrekodi walikuwa wanatumia madawa ya kulevya aina ya bangi.

Toka kwenye maji jiokoe mwenyewe utakufa“,alisema mmoja ya vijana hao na mwingine akisema “Hakuna mtu wa kwenda kumuokoa muacheni afe“, huku mwingine wa tatu akisema “Sijawahi kumuona mtu akiwa anakufa Mungu wangu inastaajabisha amezama?“, na kisha wote kumalizia kwa kutukana na kucheka.

Hata hivyo Polisi wamesema baada ya kufanya mahojiano na vijana hao wamedai walimwambia asiingie kwenye bwawa yeye aliwakatalia na walijua ni mzaha mpaka alipozama kabisa.

Taarifa kutoka kwenye familia yake zinadai marehemu siku ya tukio alikosana na mpenzi wake na alienda bwawani hapo kupumzika kwani ni eneo ambalo wakazi wa mji huo wamezoea kukaa nyakati za jioni.

Mwili wa Dunn ulikaa kwenye bwawa kwa siku tatu bila kupatikana kutokana na kuzama chini kwenye matope.

Watu wengi wanaharati nchini Marekani wameguswa na tukio hilo na kushinikiza mahakama kuwachukulia adhabu ili iwe fundisho kwa vijana wengine kwani kutokufanya hivyo kutapelekea nchi kukuza vijana wasio na maadili.

Tazama video vijana hao walivyokuwa wanamrekodi mwenzao akizama huku hao wakishangilia.

https://youtu.be/Vhng_vQW1jc

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents