Michezo

Wambura ashindwa rufaa, kuendelea kutumikia kifungo cha maisha

Kamati ya rufaa ya maadili ya TFF imetupilia mbali rufaa ya Michael Wambura aliyekuwa makamu wa Rais wa TFF ambaye alifungiwa maisha kujihusisha na shughuli za soka.

Baada ya kupitia hoja zake za rufaa, kamati ya rufaa ya maadili imejiridhisha na maamuzi ya awali yaliyotolewa na kamati ya maadili kumfungia maisha Michael Wambura.

Awali Kamati ya Maadili ya TFF imfungia kiongozi huyo kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013 baada ya kupatikana na kosa la kupokea fedha za Shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya Shirikisho.

“Kamati imejiridhisha bila ya shaka kuwa vitendo vilivyofanywa na Ndg Wambura vinashusha hadhi ya TFF, kuingiza FAT na baadae TFF katika mkopo wa Dola elfu 30 za kimarekani bila ya kufuata taratibu zozote zilizopo kwani kufanya hivyo ni ukiukwaji mkubwa na kulipaka matope Shirikisho mbele ya Umma”, ilimesema Kamati ya Maadili.

Pamoja na hayo, Kamati ya Maadili ya TFF imeendelea kwa kusema “baada ya kupitia vifungu mbalimbali vya kanuni za maadili ya TFF, na kuridhika kusipokuwa na shaka Kamati imemfungia Michael Wambura kifungo cha kutojihusisha na mpira wa miguu maisha ambapo adhabu hii imetolewa kulingana na uzito kwa kesi yake kwa mujibu wa kifungu cha 73(1) (c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013”.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents