Habari

Wanaume 1,500 kufanyiwa tohara Bariadi

Zaidi ya wanaume 1,500 wilayani Bariadi mkoani Simiyu wanatarajia kufanyiwa tohara ili kujikinga na maambukizi ya magonjwa mbalimbali kwa asilimia 60.

Hatua hiyo imetokana zoezi lilofanywa na madaktari bingwa kutoka katika Tasasi ya Kiislamu ya The Islamic Foundation kwa ushirikiano na kampuni ya ununuzi wa zao la pamba Alliance Ginnery linalofanyika katika kijiji cha Kasoli na vijiji jirani wilayani humo.

Wakizingumza katika zoezi hilo la upimaji afya na kupatiwa matibabu bure wananchi hao wanaeleza kuwa hatua hiyo ni nzuri kwao kwani wengi wao wamekuwa wakishindwa kumudu gharama za matibabu katika vituo vya afya na kusababisha kukosa huduma hiyo.

Mratibu wa mpango afya salama na mtoto wilayani Bariadi, Pamela Charles amesema sehemu zote ambazo wanaume hawajafanyiwa tohara lipo tatizo kubwa kwa akina mama walioolewa kupata tatizo la shingo ya kizazi na kwamba ujio wa huduma hiyo utasaidia kupunguza tatizo hilo ambapo ametoa wito kwa wanaume kujitokeza kwa wingi.

Kaimu Mkurugenzi wa Islamic Foundation, Mbaraka Saidi amesema lengo la kutoa huduma hiyo ni kuwafikishia huduma ambazo wengi wamekuwa hawazipati kwa muda muafaka hali ambayo imekuwa ikiwalazimu kutembea umbali mrefu.

Mbali na kutoa huduma ya tohara pia madaktari hao wamefanya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi,tezi dume na magonjwa mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa miwani bure kwa wagonjwa wa macho.

Chanzo:ITV

By Godfrey Mgallah

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents