Habari

Wanaume waagizwa kutokimbia mimba

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamisi Kigwangalla amewaagiza wanaume wanaowapa mimba wanawake kutunza mimba hizo na kulea watoto na si kukimbia na kujitokeza baada ya mtoto kuzaliwa.

Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma alipo kuwa akijibu swali la Mbunge wa Chakwa, Bhangwaji Meisuria (CCM) ambaye alitaka kujua baba ataipata wapi haki ya kumwona mtoto endapo wazazi wametengana.

“Kifungu cha 26(i) kimeeleza haki za mtoto endapo wazazi watakuwa wametengana, haki hizo ni pamoja na kuendelea kupewa matunzo pamoja na elimu kama ilivyokuwa kabla ya wazazi kutengana, kuishi na mzazi mmoja wapo baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa mzazi huyo anao uwezo wa kumlea mtoto huyo,” alifafanua.

“Ninapenda kulifahamisha Bunge kuwa zipo taratibu za kufauta endapo mzazi mmoja atakosa haki ya kumwona mtoto wake. Kwa mujibu wa taratibu mlalamikaji anaishi na mtoto ili waweze kukutanishwa na kufanyiwa unasihi ili hatimaye waweze kufikia makubaliano ya pamoja ya kumlea mtoto,” alisema Kigwangalla.

Aidha Dk Kigwangalla alisema Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009 imezingatia suala zima la utoaji wa malezi, matunzo na ulinzi wa mtoto.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents