Habari

Wanawake nchini Saudia Arabia, kuanza kupewa talaka kupitia ujumbe wa simu

Sheria mpya nchini Saudia inawalinda wanawake kutopewa talaka bila kujua. Kuanzia siku ya Jumapili , mahakama zitatakiwa kuwaelezea wanawake kupitia njia ya ujumbe wa simu kwamba wamepewa talaka.

Kwa mujibu wa BBC, Mawakili wanawake wanapendekeza kuwa hatua hiyo itamaliza kile kinachotajwa kuwa talaka za siri – ambapo wanaume hutoa talaka bila kuwaelezea wake zao.

Amri hiyo itahakikisha kuwa wanawake wanajua hali ya ndoa yao na itawalinda dhidi ya masurufu.

Mwaka uliopita marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa na mahakama nchini Saudia.

Hatahivyo wanawake bado wako chini ya usimamizi wa wanaume.

Saudi women (shown here arriving at the Janadriyah festival of Heritage and Culture in Al-Thamama, a village north of the Saudi capital, Riyadh, on Feb. 22) still need the permission of male relatives to travel and even receive certain medical procedures. But a growing number are entering the workforce.

”Sheria hiyo mpya itahakikisha kuwa wanawake wanapewa haki zao za masurufu wakati wanapopewa talaka”, alisema wakili Nisreen al-Ghamdi.

Pia ina hakikisha kuwa uwezo wowote utakaotolewa na mahakama hautumiki vibaya.

”Wanawake wengi wamewasilisha malalamisihi yao katika mahakama za rufaa kwa kupewa talaka bila ya wao kujua” , kulingana na wakili Samia al-Hindi.

Hatua hiyo mpya inasemaekana kuwa miongoni mwa mabadilikio ya kiuchumi na kijamii yalioshinikizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ikiwemo kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani na kutazama mechi za kandanada mbali na kufanya kazi ambazo awali zimekuwa zikifanywa na wanaume pekee.

Kuna vitu vingi ambavyo wanawake wa Saudia bado hawaruhusiwi kufanya bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa wasimamizi wao wa kiume kama vile waume zao , baba zao ndugu wa kiume ama watoto wao.

Vitu hivyo ni:

  • Kuwasilisha maombi ya pasipoti.
  • Kusafiri katika mataifa ye kigeni.
  • Kuolewa
  • Kufungua akaunti ya benki.
  • Kuanzisha biashara
  • Kuondoka jela

Hali hiyo ya kusimamiwa na wanaume imesababisha taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa ambayo usawa wa kijinsia umekandamizwa mashariki ya kati.

By Ally Juma.



Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents