Habari

Warundi rudini Burundi, nyumbani kuna amani – Nkurunziza

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amewataka wakimbizi wa Burundi waliopo nchini Tanzania kurundi nchini kwao kwa kuwa kwasasa kuna amani.

Rais Nkurunzinza ameyasema hayo leo katika uwanja wa mpira wa Lemela Wilaya Ngara Mkoani Kagera ambapo yupo na Mwenyeji wake Rais Magufuli.

“Ninacho taka kuwaambia Warundi warudi nyumbani tujenge Burundi yetu kwani saizi kuna amani, tunamshukuru Mwenyezi Mungu leo tumepata nafasi ya kuja kuwasilimia wenzetu Tanzania. Tunawaomba Watanzania mje kufanya biashara Burundi kama unaingia nyumbani kwenu,” amesema Nkurunziza.

“Tunataka ushirikiano kati ya Warundi na Watanzania, tutapata matunda ya kufanya kazi pamoja na matunda mtaanza kuyaona na siasa nzuri ya maisha mazuri, tunashukuru Muheshimiwa Rais kwa kutupokea Warundi.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents