Soka saa 24!

Wasanii 300 kwenda kushuhudia ujenzi wa reli ya Kisasa ‘SGR’ (Video)

Wasanii takribani 300 nchini Tanzania wanatarajiwa kutembelea mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Januari 5, 2019 na mratibu wa safari hiyo, Steve Nyerere wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema katika safari hiyo watakuwepo wasanii wa Bongo Fleva, muziki wa dansi, singeli, filamu, wachezaji wa mpira wa miguu, washereheshaji na wachezaji wa mpira wa kikapu.

Amebainisha kuwa safari hiyo ni matokeo ya kikao walichoketi wiki iliyopita na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema safari hiyo itaanza saa  1 asubuhi eneo la Kamata na kupita katika maeneo ambako ujenzi unaendelea.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW