Burudani

Wasanii: Tamasha la siku ya muziki duniani ni njia panda ya Ulaya

Wanamuziki walioshirika katika tamasha la siku ya muziki duniani lililofanyika siku ya Ijumaa wiki iliyopita kwenye viwanja vya posta jijini Dar es Salaam wamesema jukwaa hilo ni njia panda ya Ulaya itakayowawezesha kupata maonyesho makubwa ya kimataifa.

Mwanamuziki-wa-HipHop-Godzilla
Godzilla alikuwa miongoni mwa wasanii waliotumbuiza

Katika maoni yao juu ya ushiriki wao katika tamasha hilo wanamuziki hao wamekiri kukua kwa muziki wa Tanzania na kukubalika kimataifa jambo ambalo katika kipindi cha miaka ya nyuma ilikuwa ni changamoto kubwa.

Mshindi wa tuzo tatu za Kilimanjaro Music Award 2012, Kala Jeremiah analielezea onyesho hilo kama mwanza wa mafanikio ya kupata matamasha mengi ya kimataifa hasa katika wakati huu ambao ameibuka msanii bora wa Hip Hop.

IMG_4290
Kala Jeremiah

“Nimepata faraja sana kualikwa kutumbuiza kwenye siku ya muziki duniani, inaonyesha ni kwa jinsi gani muziki wangu unakubalika na kutambulika kitaifa na kimataifa”

Anasema kuwa pamoja na mashairi ya muziki wake kuwa katika lugha ya Kiswahili anamatumaini makubwa ya kuliteka soko la muziki la kimataifa kwakuwa mataifa mengi sasa yanawafuasi wengi wanaopenda kiswahili na kukisapoti.

Mkali wa mitindo huru nchini Godzila anasema tamasha hilo limemkutanisha na hadhira mpya ya kimataifa na anaamini kutakuwa na mikataba mingine ya kufanya matamasha kama hilo nchi za nje.

“Miongoni mwa mafanikio ya mwanamuziki ni kupata matamasha ndani na nje ya nchi yake, kupitia tamasha hilo naamini nitapokea mialiko ya kufanya maonyesho ya kimataifa” anasema Godzila.

Naye Mkali wa R&B Ben Paul anajivunia uwezo wake akiamini kuwa ndio umemwezesha kutambulika na kukubalika katika jamii ya watu wa mataifa mengine jambo ambalo hata wakati akitumbuiza jukwaani wazungu hawakuwa nyuma kuimba nyimbo zake.

Benpol-akiimbamba-katika-siku-ya-muziki-duniani-iliofanyika-pale-vyiwanja-vya-kijitonyama-leo.

“Nimekutana na watu wanaopenda muziki wa r&b na kiswahili kinapendwa asikwambie mtu, unaona hata hao wazungu wameimba pamoja nami” anasema Ben Paul.

Mashabiki nao walitoa yao juu ya tamasha hilo ambapo Silas Mbuya anasifu jitihada za taasisi mbalimbali nchini kukuza na kuendeleza muziki wa Tanzania kwa kuandaa matamasha ya aina hiyo.
Mratibu wa tamasha hilo Abel Shuma ambaye pia ni Mratibu wa Shughuli za Utamaduni Alliance France Dar es Salaam anasema “Siku ya muziki duniani ni fursa ya kutangaza na kukuza muziki na utamaduni wa nyumbani katika jukwaa la kimataifa”

Anasema kuwa wanamuziki walioshiriki tamasha hilo wananafasi kubwa ya kupata mialiko ya kufanya maonyesho katika nchi za ulaya na mataifa mengine uliwenguni kwa kuwa limewakutanisha pia mapromota wa muziki kutoka nchi mbalimbali.

Tamasha hilo liliandaliwa na umoja wa ulaya wa taasisi za utamaduni (EUNIC) na kudhaminiwa na Fastjet, Pepsi, Total na balozi za Ujerumani na Ufaransa.

Imeandikwa na Dotto Kahindi

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents