Burudani

Wasanii wa zamani tulilemazwa na single kujipromote zenyewe – Jaffarai

Jaffarai anaamini kuwa wasanii wa zamani walilemazwa na muziki wa kipindi hicho kwakuwa ulikuwa unaenda wenyewe tofauti na sasa hivi.

Jafarai

Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo Beats cha Star TV, Jaffarai alisema kwa sasa muziki umebadilika na kuwa ni zaidi kipaji.

“Zamani mimi nilikuwa label pale Bongo Records, nyimbo yangu ya Nipo Busy sijaipeleka redio,” alisema. “Zamani ulikuwa ukishaisha studio umemeliza, utasikia tu nyimbo inapigwa Clouds, inapigwa East Africa, yaani kila radio utasikia inapigwa. Unajiuliza ile imefikaje kule kumbe inapelekwa na maproducer wenyewe wanazituma,” aliongeza.

“Kwahiyo zamani wasanii hawakuwa wanapata tabu, ilikuwa ni rahisi tu kuimba nyimbo kali inaenda, anakuja mtu wa video unafanya hutoi hata hela, mtu anakuja anachukua DVD zako zinauzwa unapewa tu pesa. Ile hali ililemaza sana watu, kwa sababu vitu vilikuwa vinaenda vyenyewe.

Sasa hivi mtu ukiwa na kipaji peke yake unafeli. Hata industry imebadilika inahitaji mambo mengi. WasAnii wamekuwa wengi, muziki wa sasa hivi unaHitaji update kila sehemu. Lakini zamani vitu vilikuwa vinaenda vyenyewe automatic. Kwakuwa tulishazoa ile hali vitu vimebadilika sasa hivi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents