Habari

Washindi wa Multichoice Talent Factory waja filamu mbili za moto, kuanza kuoneshwa DSTV (Video)

WAHITIMU wa mafunzo maalum ya uzalishaji filamu chini ya programu ya Kampuni ya Multichoice talent factory wajipanga kuleta mapinduzi kwenye soko la filamu duniani.

Filamu hizo zimesimamiwa na kuzalishwa na kijana hao kutoka Tanzania aliohitimu MultiChoice Talent Factory Academy inayoelezea maisha ya dereva bodaboda na mkewe waliopitia misukosuko kibao maishani mwao.

Akizungumza na waandishi wahabari wakati wa kutambulisha rasmi filamu mbili zilizotengenezwa na wahitimu hao Wilson Nkya amesema wanapongeza uongozi wa Multichoice kwa kuendelea kukuza vipaji vya vijana wenye ndoto za kufanya vitu vikubwa katika sekta ya filamu.

“Mafunzo tuliyotapata yameweza kutupa akili na maarifa jinsi gani tunateweza kutengeneza filamu bora zenye kujenga jamii na kutumia vitu asilia vya kutambulisha utamaduni Kama vile maporomoko ya maji,ngoma za asili na vitu vyenye upekee ,”

Aidha ameeleza pia kwa kipindi chote cha mafunzo wameweza kuandaa filamu mbili Ensulo pamoja na promise ambazo zitarusha hivi karibuni kupitia King’amuzi cha dstv kupitia Maisha magic bongo.

Na pia miongoni mwa wahitimu hao Janet Moshi amesema pamoja na kupatiwa na mafunzo hayo bado wanania ya dhati kubadilisha soko la filamu kuanzia utengenezwaji wa miswada (Script) ,kuongoza filamu pamoja kutengeneza picha jongefu.

” Wasanii na waongozaji (directors) wanatakiwa kujifunza kutengeneza filamu kwa kutumia bajeti ndogo pamoja na kutumia vitu ambavyo vinaweza kueleweka kwa urahisi kwa watazamaji,”

Usikose kuona uwezo mkubwa wa vijana wetu waliokuwa kwenye Academy hiyo. Ni Ijumaa hii 20 Septemba saa 12 jioni kupitia DStv chaneli 160 pekee!. Lipia kifurishi 19000 tu kujiunga na DStv au piga 0659070707

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents