Burudani

Watayarishaji wa muziki wa siku hizi hawapati kitu – Master J

Mtayarishaji mkongwe wa muziki Master J, amefunguka kwa kudai kwamba watayarishiji wa muziki wa siku hizi hawalipwi vizuri tofauti na awali.

Master J ameiambia EFM kwamba kuna watayarishaji wengi wahalipwi vizuri kuliko wale ambao wanalipwa vizuri kidogo.

“Maproducer wengi hawapati kitu, yaani msanii akikuheshimu sana atakupa laki mbili au laki tatu lakini hawa wengine wote ni laki kushuka chini wimbo mzima mpaka beat,” alisema Master J.

Katika hatua nyingine mtayarishaji huyo amewataka wenzake kuacha ku-copy kazi za nje ambazo zinaenda kuharibu asili ya muziki wa Tanzania.

“Kiukweli Muziki wetu umepoteza uhalisia tunakopy sana kutoka kule Nigeria, Maproducer waongeze ubunifu kidogo ili tuweze kuwa na aina ya Muziki wetu . Kwa maana hili sio zuri maana tuna makabila Zaidi ya 120 tunaweza kuchanganya na kupata uhasilia wetu” alisema Master J.

Mtayarishaji huyo kwa sasa amesimama kuandaa muziki kwa madai amewaachia vijana wapya na wao wafanye wanachokiweza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents