Burudani

Waters Up ya Lucci ft Jokate na Julio wavunja rekodi kwa kuwa wimbo uliodownlodiwa zaidi mwaka huu

Haisikiki sana kwenye radio kama nyimbo zingine zilizotoka mwaka huu lakini amini usiamini, Waters Up ya Lucci ft Jokate na Julio ndio wimbo ulioshushwa (downloaded) zaidi kuliko zote zilizotoka mwaka huu.

Kupitia akaunti ya Hulkshare ya Dj Choka, Waters Up imeshushwa mara 30,095 na kusikilizwa mara 13,179 tangu uwekwe tarehe 2 mwezi uliopita wakati kwenye akaunti Michael Mlingwa ya mtandao huo wa kuhifadhia nyimbo (file sharing site) ngoma hiyo imeshushwa mara 27,327 na kusikilizwa mara 4,137.

hugoline downloads

mx carter downloads

Kupitia maelezo yaliyotumwa na Lucci pamoja na uongozi wa studio yake TransforMaX Records, takwimu hizo hata wao zimewaacha mdomo wazi.

“Team nzima ya TransforMaX Records inayomilikiwa na producer Lucci ingependa kutoa shukurani kwa kila mtu aliye support wimbo wa “waters up” kwa namna moja au nyingine. Ama kweli ukitaka kujua wimbo una demand kubwa, usiangilie Air Play ya radio bali idadi ya downloads. Downloads humaanisha watu wanataka kuwa nao wimbo wakati wote. Ndani ya mwezi mmoja tu wimbo wa “waters up” umeweza kupata downloads zaidi ya 50,000 kupitia mtandao wa hulkshare.

Lucci
Lucci

Mimi kama Lucci nasema ahsante kwa blogs zote, contacts wangu wote na kila mtu ambaye alikua akisambaza link hii na nyinginezo.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents