Habari

Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wameogopa ushindi wa kisulisuli – Polepole

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema kuwa watu wa vyama vya upinzani ni waungwana sana kwakuwa wameamua kujitoa wenyewe kwenye mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, baada ya kukiona chama hicho kilivyo imara na hawawezi kushindana nacho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole

Polepole amesema hayo leo Novemba 13, 2019, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Watu wa vyama vya upinzani ni waungwana, wametazama wakasema mambo yatakayotokea kwenye uchaguzi huu si ya mchezo, kwetu sisi ile 2014 inawezekana ulikuwa ushindi wa Tsunami ila wa mwaka huu utakuwa ni ushindi wa kisulisuli na ndiyo maana wakaamua kabla hatujafika pabaya wakaweka mpira kwapani”, amesema Polepole.

Aidha Polepole amevitaka vyama vya upinzani kujifunza kulingana na historia iliyopita kwakuwa kuna baadhi ya maeneo hawana wafuasi kabisa kama ilivyo CCM.

“Wanasema historia ni somo la kale la sasa na linakusaidia kuutazama wakati ujao, vyama vya siasa vijifunze makosa ya leo, wamefanya tathmini ya makosa ya 2014?. tasingizia mikutano ya hadhara, kila chama kinafanya mikutano kwa mujibu wa utaratibu tuliojiwekea lakini wenzetu kwenye maeneo yao hawafanyi.”, ameongeza.

Hadi kufikia leo Novemba 13, 2019, jumla ya vyama 7 vya upinzani, vimekwishajitoa katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa kile walichokieleza kuwa hawajatendewa haki baada ya majina ya wagombea wao kuenguliwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents