Habari

Waziri Mkuu apigilia msumari suala la chakula kutoka nje

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameendelea kusisitiza kuwa hakuna chakula kutoka nje ya nchi hususani Mahindi.

Waziri Majaliwa ametoa msisitizo huo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Ritta Kabati (CCM) aliyetaka Serikali iruhusu kusafirisha mahindi nje ya nchi.

“Suala hili nililizungumzia kwenye Baraza la Eid kule mjini Moshi mkoani Kilimanjaro na nilizungumza kwa msisitizo kwamba tumedhibiti na tumezuia usafirishaji wa chakula na hasa Mahindi nje ya nchi, kwasababu historia yetu sisi kuanzia mwaka jana mwezi Novemba mpaka Februari mwaka huu nchi yetu ilikosa ilikosa mvua za msimu inavyotakiwa na tukapata usumbufu mkubwa ndani ya nchi kwa maeneo mengi kukosa chakula cha kutosha,” alisema Majaliwa.

“Lakini kwasasa naona chakula kikuu Tanzania, na naona utamaduni umebadilika Wachaga,Wahaya baada ya kula ndizi sasa wanakula ugali, wamasai waliokuwa wanakula nyama tu sasa wanakula ugali kwahiyo unakuta mahindi yanatumika sana kuwa ni chakula kikuu kwahiyo ni lazima tuweke udhibiti wa mahindi ili yaendelee kutusaidia kama chakula kikuu hapa nchini kwetu kwahiyo tumeweka zuio.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents