Habari

Waziri Mkuu atoa kauli hii kuhusu usalama wa nchi

Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali haitafumbia macho vitendo vya kuhalifu vinavyoendelea katika maeneo mbalimbali nchini huku akiwataka wabunge kuwa wavumilivu wakati vyombo vya dola vikichukua hatua stahiki kudhibiti vitendo hivyo.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Bungeni mjini Dodoma alipowasilisha hotuba yake ya kuahirisha Mkutano wa Nane wa Bunge.

“Nitumie fursa hii kusisitiza kwamba kwa matukio haya serikali haitafumbia macho, tayari vyombo vya dola vimeombwa kuhakikishja kwamba zinawatafuta kwa mbinu zote wale wote wanaohusika na vitendo hivyo,” alisema waziri.

“Nirejee kuwaambia wabunge wenzangu na watanzania wote waendelee kuvuta subira wakati vyombo vya dola vinashughulikia matukio haya kwa umakini mkubwa,” aliongeza.

Bunge limehairisha mpaka tarehe 7 Novemba mwaka huu saa 3 asubuhi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents