Habari

Waziri Mkuu ausifia mfumo wa tiketi za kieletroniki uwanja wa taifa

Serikali imepongeza ufanisi wa tiketi za kielektroniki katika viingilio vya uwanjani baada ya mwishoni mwa wiki mashabiki kuingia uwanjani kwa kutumia njia hiyo.

waziri-mkuu-kassim-majaliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliingia uwanjani hapo kushuhudia michezo miwili ya hisani ya soka iliyohusisha pia wabunge.

“Kwa mfumo huu sasa uwanja wetu wa taifa unaanza kukusanya fedha inayokusudiwa ili tuweze kuvigawia vilabu ambavyo tunalenga vinufaike. Meneja wa uwanja mwenyewe aweze kupata fungu zuri la uhakika, kwa ajili ya maintenance ya uwanja wenyewe na huduma nyingine zote ziweze kukaa vizuri,” alisema Majaliwa

“Kwahiyo nimefurahi kuona tayari tumejenga mfumo,unafanya kazi na nimetest leo mfumo unafanya kazi. Mheshimiwa spika kapita kaweka mfumo na mheshimiwa waziri tunataka kila mmoja kwa wadhifa wake lazima apite kwenye kiwanja chetu kwa kadi,” aliongeza.

Hivi karibuni waziri wa habari, utamaduni,sanaa na michezo, Nape Nnauye alizindua mfumo huo wa kielektroniki na kushuhudiwa na waandishi wa habari za michezo.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents