Habari

Waziri Mkuu awataka Watumishi wa umma kutojihusisha na rushwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka Watumishi wa Umma nchini kutojihusisha na vitendo vya rushwa katika utoaji wa huduma kwa Wananchi.

Waziri Mkuu ameyasema hayo Jumatatu hii, wakati akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Liwale katika Ukumbi wa Tengeneza.

Waziri Mkuu ambaye yuko katika na ziara ya kikazi ya siku nne Mkoani Lindi, alisema Watumishi wanawajibu wa kuwahudumia wananchi bila ya kutengeneza mazingira ya kuomba rushwa na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Aidha Waziri Mkuu alisema watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia maadili ya kiutumishi jambo litakaloondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.

“Lazima wananchi waone na wanufaike na kazi inayofanywa na Serikali yao, hivyo ni wajibu wa watumishi kuwatumikia wananchi popote walipo na si kukaa maofisini,” alisisitiza Waziri Majaliwa.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents