Habari

Waziri Nchemba atoa agizo kuungua kwa soko Mbeya

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza jeshi la zimamoto na Uokoaji na kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mbeya kuchunguza wa kina juu ya chanzo cha kuungua soko la Sido lililopo mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ambapo ametoa rai kwa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la Zimamoto wakati wa ujenzi ili kuweka miundombinu itakayoweka shughuli za uokoaji.

“Uchunguzi ufanyike kuhusu ni vyanzo vya matukio ya moto ambavyo vimeanza kujitokeza na naelekeza maeneo mengine yote kuchukua tahadhari kufuatana na mazingira yao kuhusu masuala haya ya moto yanayoweza kujitokeza yanatupozea mali za watu lakini pia ni matukio ya hata yanayoweza kutugharimu zaidi hata ya hizo mali zitakazo weza kujitokeza,” alisema Nchemba.

“Zaidi nitoe lai kwa halamashauri ambapo taratibu za ujenzi zinafanyika, mar azote wanapofanya shughuli za ujenzi wahakikishe wanashirikiana na mamlaka ya zima moto ili kuweka kwenye mpangilio matarajio ya namna vifaa vya uokoaji vinavyoweza kupita punde yanapotokea matukio kama haya,” aliongeza Waziri Nchemba.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents