DStv Inogilee!

Wedding Bells: Paul Okoye (P-Square) kufunga ndoa hivi karibuni

Kuna habari kuwa Paul Okoye wa kundi la mapacha wa P-Square wa Nigeria, yuko mbioni kuachana na kambi ya ukapela kwa kufunga ndoa na mpenzi wake aitwaye Anita anayefanya kazi kwenye kampuni ya mafuta.

Japo Paul amekuwa mkimya kuhusu mipango hiyo, watu wa karibu wanasema anaweza kufunga ndoa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa vyanzo vya nchini Nigeria, marafiki wa karibu na Anita wanadai kuwa hicho ndicho kitu pekee anakifuatilia kwa sasa.

Vyanzo hivyo vimesema Paul anajulikana kwa kila ndugu wa mpenzi wake huyo na hata wazazi wake wamependa chaguo lake la mume.

Inadai kuwa Paul amekuwa akimpa good times mrembo huyo kwa kumpeleka nchi za nje, zawadi, pesa na vitu vingine vilivyofanya adate!

Pacha wake Peter tayari ana familia yenye mtoto mmoja na wanatarajia kupata mtoto mwingine miezi kadhaa ijayo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW