Burudani

Wema alioutenda Mwana FA kwa Dj Choka

By  | 

Dj Choka ameelezea jinsi msanii wa hip hop, Mwana FA alivyokuwa msaada kwake mara baada ya hali yake kiafya kubadilika walipokuwa safarini wakitokea mkoani Tanga.


Kupitia mtandao wa instagram Dj Choka ameandika, “Nikiwa sijui kitanitokea nini, baada ya kumaliza show ya Handeni -Tanga kusherehekea mwaka mpya 2017. Tukiwa tunarudi Dar tarehe 2 January nikiwa kwenye gari mimi na braza Mwana FA ndipo nikaanza kukooa damu mafundo matatu.

“Sikujua ni kitu gani huku tukijiuliza labda ni nyongo au kuna tatizo kwenye koo la hewa. Ndipo ikabidi Mwana FA akimbize gari kuwahi hospitali za Dar maana tulikuwa tumeshaingia barabara ya Msata to Bagamoyo,” aliongeza.

“Tulifika Dar es Salama na kuwahi hospitali ya Marie Stoper na baadae nikaelekezwa niende Hospitali ya Kairuki kwa vipimo zaidi. Kesho yake tarehe 3 nikashauriwa kwenda Mwananyamala hospitali na hapo nilipata vipimo haraka kwa kupima Mapafu na ndipo nikagundulika nina KifuaKikuu(Tuberculosis) na kuanza dozi yake ya miezi 6 kwa Haraka,” ameandika Dj Choka.

By Peter Akaro

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments