Burudani

Wema Sepetu atoa jibu juu ya shepu yake

Ikiwa ni wiki imepita tangu malkia wa filamu Bongo Wema Sepetu, kuposti picha kadhaa katika mtandao wa kijamii wa Instagram kuonesha umbo lake, mwana dada huyo ameamua kuwajibu wale wanaodhania shepu hiyo sio yake.

Wema ambaye kwa sasa hataki kujihusisha na skendo yoyote ameandika “Shepu ya mwendokasi… Ndo niliojaliwa nayo… Kama imeanzia kiunoni kwenda magotini ndo niliojaliwa nayo… Kama wewe hauna basi mshukuru Allah… Ndo nilivyoumbwa jamani… Sio mimi bali ni Maulana ndo alionibariki nayo… Hata ingekuwa kwanzia kichwa hadi Vidole vya miguuni ni sawa pia… Ndo niliojaliwa nayo.”

“Sometimes najiangalia kwenye kioo sijimalizi… Ndo majaliwa yangu… Ndo yangu basi… Imenizidia… Allah Subhanah wataallah ndo amenipa… Aaaah….!? Sio shepu ya kawaida… Niacheni na Shepu yangu jamani… Ndo nishaimiliki mie… Siwezi kuitoa…. ????,” ameandika mrembo huyo.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents