Burudani

Weusi wajifunza mambo haya kutoka kwa Future: Waahidi pia kuachia kolabo yao na Sauti Sol (+Video)

Kundi maarufu la Muziki la Weusi Kampuni limeahidi kuachia Kolabo yake ya kwanza kufanya na kundi la Sauti Sol kutoka nchini Kenya.

Weusi wamesema kwa sasa wameshafanya kolabo na Sauti Sol kinachosubiriwa ni vitu vichache tu kumalizika ili waweze kuachia Kolabo hiyo.

Hata hivyo, Weusi wamethibitisha kuwa kuna Kolabo nyingine mbali na hiyo ya Sauti Sol ambazo wamefanya na Rapa Falz na YCEE wote kutoka Nigeria.

Kwa upande mwingine Weusi wanaotamba na single yoa ya ‘ Naliamsha Dude’ wamesema wamejifunza vitu vingi kikiwemo uzoefu wa kuperfom kwenye majukwaa ya kimataifa hii ni baada ya kuona Perfomance ya Rapa Future.

Tazama mahojiano ya Weusi hapa chini.

Weusi, Vanessa Mdee, Navy Kenzo na Diamond Platnumz ndiyo Wasanii pekee kutoka Tanzania ambao walipata bahati ya kutumbuiza kwenye tamasha la Castle Light Unlocks lililofanyika jana usiku kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es salaam ambapo Rapa wa kimataifa kutoka Marekani, Future alitumbuiza pia.

By Godfrey Mgallah 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents