Habari

Wewe kuwa jaji: Unamkubali Adam Mchomvu kama rapper?

Hakuna ubishi kwamba Adam Mchomvu aka Baba Jonii wa Clouds FM ni miongoni mwa watangazaji wa vipindi vya burudani maarufu nchini Tanzania. Lakini pamoja na kuwa mtangazaji, Adam ni rapper pia na tayari amewahi kuachia track kibao ambazo hata hivyo nyingi huishia kuchezwa kwenye kituo cha radio anachofanyia kazi pekee. Radio zingine tunahisi kama bado hazijamuelewa hivi ama vinabana tu!

Hivi karibuni mtangazaji mwenzie B12, alimpa changamoto na kumwambia kuwa nyimbo zake hazioneshi userious na zimekuwa za aina moja (kitoto) huku akidai kuwa kama asingekuwa Clouds nyimbo zake zisingechezwa kabisa.

Yeye mwenyewe anajua kuwa bado wananchi hawajamuelewa vizuri licha ya kusisitiza kuwa Hip Hop ndio maisha yake.

“Babajonii kwa booth … Tutaelewana TU japo raiaa wanajifanya hawaelewi sömo,” ameandika leo kwenye ukurasa wake wa Facebook akiambatanisha picha inayomwonesha akiwa kwenye chumba cha kuingizia sauti.

So tunataka wewe uwe Jaji, unamkubali Adam kama rapper?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents