Habari

Wizara yaeleza sababu za wanawake kuathirika zaidi na VVU, biashara ya ngono yatajwa

Serikali kupitia Wizara ya Afya Jinsia, Wazee na Watoto imeeleza sababu nne za kitaalamu zinazosababisha wanawake kuathirika zaidi na VVU kuliko wanaume ambapo biashara ya ngono ni moja ya sababu zilizotajwa.


Naibu Waziri wa Afya,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile

Hayo yamewekwa wazi leo bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya,Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la Mbunge wa Mtamwe, Mh. Khalifa Mohamed Issa aliyetaka kufahamu kwa takwimu zilizo inakisiwa kuwa watu wote wanaoishi na Ukimwi Tanzania ni zaidi ya milioni moja na laki tano na inaaminika kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa zaidi, Je? Ni sababu gani za kitaalamu zinazoaminika kuwa wanawake ndio waathirika zaidi kuliko wanaume?

“Sababu za kitaalamu zinazosababisha wanawake kuathirika zaidi na VVU na Ukimwi yapo kama manne na naomba niyatoe kama ifuatavyo sababu ya kwanza ni ya kimaumbile na kibiologia mwanamke yuko katika hatari zaidi ya kuambukizwa VVU ukilinganisa na mwanaume kwa kuwa maumbile ya mwanamke ni rahisi kupata mchubuko wakati wa tendo la ndoa hivyo kurahisisha virusi vya Ukimwi kupenya aidha maumbile ya mwanamke hupokea mbegu za kiume kutoka kwa wanaume wakati wa tendo la ndoa iwapo mwanamke atafanya mapenzi na mwanaume mwenye VVU mwanamke huyo anaweza kuambukizwa virusi vya Ukimwi,” amesema Dkt. Ngungulile.

Ameendelea kueleza “Sababu ya pili Mh. Naibu Spika kwamba kuna tabia na mazingira hatarishi ambayo husababisha hatari kuamukizwa VVU ikiwa ni pamoja na kufanya biashara ya ngono na kuanza mapenzi katika umri mdogo.”

“Sababu ya tatu ni mfumo dume uliopo katika jamii yetu unawapa fursa kwa wanaume kufanya ngono na wanawake wengi, kutotumia condom, kuoa wasichana wenye umri mdogo na hata kufanya ukatili wa kijinsia mfumo huu una sababisha baadhi ya wanawake kuambukizwa VVU hata kushindwa kuwaelewa hali zao maambukizi ya VVU kwa wenza wao kwa kuhofia kuachika kutengwa au kufukuzwa kutoka kwenye familia kwa kawaida mfumo dume huambatana na kuwa ubaguzi ambao pia ni kikwazo kikubwa kwa wanawake kuwa wazi kuhusu hali zao za maambukizi ya VVU na hasa kutengwa na familia zao au jamii,”ameongeza Dkt. Ngungulile.

“Na sababu ya mwisho ni kwamba wanawake wengi hujitokeza kupima, nitoe rai kwa wanaume kujitokeza kupima tusitumie wenza wetu kama kipimo cha kwetu sisi.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents