Habari

Yaelezwa Kenya yaomba kupeleka wanajeshi eneo la baharini wanalozozaniwa na Somalia

Yaelezwa Kenya yaomba kupeleka wanajeshi eneo la baharini wanalozozaniwa na Somalia

Kenya huenda ikatuma jeshi lake katika eneo la baharini inalozozania na Somalia iwapo muswada uliowasilishwa bungeni utaidhinishwa. Muswada huo uliowasilishwa na kiongozi wa walio wengi Bungeni Adan Duale na mwenzake wa walio wachache John Mbadi unataka kuishinikiza serikali kutumia mikakati mengine ya kisheria ili kulinda himaya hiyo ya Kenya ikiwemo kutuma majeshi katika eneo hilo la mpaka ili kuchukua jukumu la kulilinda.

Akitoa notisi ya muswada huo Duale amewataka wabunge kuuidhinisha muswada huo utakapowasilishwa kwa mjadala ili jeshi lichukue wajibu wake wa kulinda eneo hilo.Chini ya katiba ya Kenya, jeshi la Kenya KDF lina jukumu kuweka ulinzi katika himaya ya Kenya na linaweza kupelekwa katika eneo lolote lenye misukosuko mpakani kuweka amani kupitia idhini ya bunge.

Hatahivyo viongozi hao wamemtaka rais Uhuru Kenyatta kufanya mazungumzo na serikali ya Somalia kwanza ili kutatua mzozo huo wa mpaka kwa manufaa ya mataifa yote mawili na eneo hili kwa jumla kupitia njia za kidiplomasia.

Katika taarifa hiyo iliotiwa saini na viongozi hao wawili na kutumwa kwa vyombo vya habari, aidha wamemtaka kiongozi huyo kutumia mikakati ya kutatua migogoro iliopo katika Umoja wa Afrika, IGAD na jumuiya ya Afrika mashariki EAC kutatua mgogoro huo.

”Bunge limeamua kwamba serikali ifanye mazungumzo na serikali ya Somali ili kutatua mgogoro huo wa mpakani kwa manufaa ya mataifa yote mawili”, ilisema taarifa hiyo.

Eneo la mpaka linalozozaniwa

Vilevile viongozi hao wanamtaka kiongozi huyo wa taifa kuwasilisha pingamizi mbele ya Umoja wa Mataifa UN kwamba taifa la Kenya linapinga kwa hali yoyote uwezo wa mahakama hiyo ya kimataifa kutatua mgogoro huo.

Kwa mujibu wa BBC.Viongozi hao wamekasirishwa na hatua ya Somalia wakati wa mkutano wa wiki ya mafuta barani Afrika mjini Cape Town kwamba iko katika mkakati wa kuyaweka katika ramani yake maeneo yake yote ya mafuta kwa lengo la kuyapiga mnada .

Somalia iliandaa mkutano wa mafuta na gesi mjini London na kufichua mipango yake ya kuvipiga mnada visima vyake vya 230, 231, 232 na 233 vilivyopo katika eneo linalozozaniwa.

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo Mahakama ya haki mjini The Hague Uholanzi inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi ya mgogoro huo kuanzia tarehe tisa Septemba hadi 13.

Tayari kundi moja la wataalam wa baharini nchini Kenya wameiomba serikali kutotumia nguvu na badala yake kutumia diplomasia kwa minajili ya amani katika eneo la magharibi mwa bahari Hindi.

Je kuna athari gani iwapo Kenya itapoteza kesi hiyo?

Kundi hilo limesema kwamba iwapo Kenya itapoteza kesi hiyo kwa mahakama hiyo ya kimataifa itasalia nchi isio na bahari na italazimika kuiomba Somalia na Tanzania ruhusa kwa meli zake kuingia katika bahari ya Mombasa.

Wabunge wa Kenya

Hiyo inamaanisha kwamba kesi hiyo itaendelea licha ya Kenya kuendelea kutafuta suluhu nje ya mahakama hiyo.

Nairobi inasema kwamba kesi hiyo haikustahili kuwasilishwa katika mahakama hiyo kwa kuwa kulikuwa na njia mbadala ambazo zilikuwa hazijatumika.

Je Kenya inasemaje?

Kenya vilevile imeishutumu Somalia kwa kuendelea kutangaza mauzo ya mafuta hayo kwa wawekezaji licha ya kwamba eneo hilo bado linazozaniwa. Imesema kuwa Mogadishu imekuwa ikitumia ramani ambayo inaingilia Himaya ya Kenya.

Hatahivyo Mogadishu imepinga kauli ya kuingilia himaya ya Kenya.

Kwa nini Somali iliishtaki Kenya

Somalia ilienda katika mahakama ya ICJ ikitaka mpaka wa baharini kati yake na Kenya kuchorwa upya ili uweze kushuka chini ukipita mpaka wake wa ardhi badala ya kwenda mashariki.

Tatizo ni kwamba Kenya inasema kwamba baadhi ya makampuni yameanza kutafuta mafuta katika meneo hayo hayo yanayozozaniwa na mataifa yote mawili.

Wiki tatu zilizopita , Kenya iliwasilisha malalamishi yake kwa taifa la Norway baada ya kampuni moja ya taifa hilo kutumia ramani inayozozaniwa kubaini kiwango cha mafuta kilichopo eneo hilo.

Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta
Image captionRais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Somalia yakana kunadi visima vya mafuta vinavyozozaniwa

Somalia ilikanusha tuhuma kwamba imenadi maeneo ya mafuta yaliopo katika mpaka unaozozaniwa kati ya taifa hilo na Kenya.

Katika taarifa yake erikali ya Somalia ilisema ‘haina mipango wala haikuwa na mipango ya kufanya hivyo’.

Taarifa hiyo ilitolewa baada ya kuwepo ripoti za kikao kilichofanyika katika mji mkuu Mogadishu cha maafisa wakuu serikalini akiwemo rais mwenyewe Mohamed Abdullahi Mohamed Farmajo na waziri mkuu Hassan Ali Khayre.

“Somalia kwa sasa haina mpango wala haikuwa na mpango wa kunadi sehemu yoyote katika eneo linalo zozaniwa baharini hadi pale mahakama ya ICJ itakapobaini mipaka ya nchi husika,” ilieleza taarifa hiyo rasmi.

taifa hilo lilitoa ahadi kwa Kenya kuwa haitojihusisha katika shughuli zozote katika maeneo yalio kwenye mzozo hadi mahakama itakapotoa uamuzi wa mwisho.

Somalia imeihakikishia Kenya kuwa itasubiri uamuzi wa mwisho wa mahakama ya ICJHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSomalia imeihakikishia Kenya kuwa itasubiri uamuzi wa mwisho wa mahakama ya ICJ

Hivi majuzi Nairobi ilitangaza kuwa inamrudisha nyumbani balozi wake aliyepo Mogadishu Luteni Jenerali mstaafu Lucas Tumbo, ikidai kuwa uamuzi wa Somalia kupiga mnada eneo moja la mafuta mjini London si sawa na uchokozi dhidi yake na mali yake asili.

Vilevile Nairobi ilimrudisha nyumbani balozi wa Somalia nchini Kenya Mohamed Nur katika kile ambacho serikali ya Kenya baadaye ilifafanuwa kwenye vyombo vya habari nchini kuwa ni kutoa fursa ya majadiliano ya kila upande katika suala hilo.

‘Kwa kupuuza suluhu ya sheria za kimataifa kuhusu mipaka ama makubaliano ya kisiasa kupitia diplomasia , serikali ya Somalia imeonyesha wazi bado haijakomaa kisiasa” , amesema katibu wa maswala ya kigeni nchini Kenya Macharia Kamau.

Eneo linalozozaniwa linakisiwa kuwa na mafuta na gesiHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionEneo linalozozaniwa linakisiwa kuwa na mafuta na gesi

Mambo 3 makuu yanayohatarishwa kwa mvutano huu

Kumeshuhudiwa mvutano na malumbano kuhusu mipaka baina ya mataifa hayo mawili katika siku za nyuma.

Baadhi ya wachambuzi wanaona kwamba hili ni jambo lisilohitajika kwa sasa.

Na huenda ni jambo ambalo mataifa yote mawili yanalitambua kutokana pia na kauli ya Somalia kwenye taarifa yake jana ya kukanusha madai hayo ya kupiga mnada mafuta na gesi katika eneo hilo linalozozaniwa, kwa kukiri kwamba ‘mataifa hayo “yameshikana katika namna ambayo hayawezi kuvunjika” na kuwa yana uhusiano mzito wa kihistoria na kitamaduni, ambayo Somalia haitaki kuuvunja.

Wafanyibiashara wa Miraa

Mchambuzi wa masuala ya Afrika, Ibrahim Aidid, anasema Kenya na Somalia ni mataifa ambayo yameweza kufanya vitu vingi kwa pamoja na kwa ushirikiano mkubwa.

Mataifa hayo mawili yamekuwa yakishirikiana katika masuala ya:

Usalama:

Kenya inategemea ushirikiano mkubwa kutoka Somalia katika vita dhidi ya ugaidi, hususan dhidi ya kundi la wapiganaji wa Alshabaab, ambalo ni tishio sio tu kwa mataifa hayo mawili, lakini pia kieneo.

Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka mataifa mengine kama Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya mwamvuli wa kikosi cha kulinda amani Amisom, wamekuwa wakiisaidia serikali ya Somalia katika vita hivyo.

Wanajeshi wa Kenya waliingia Somalia mnamo mwaka 2011, kuwapiga vita wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa al-Qaeda.

Biashara:

‘Kenya inapeleka biashara Somalia. Imenufaika pakubwa kifedha kwa bidhaa kwa mfano kama miraa zinazosafirishwa hadi Somalia’, anasema mchambuzi wa kisiasa Ibrahim.

Usafirishaji wa miraa au mirungi hadi Mogadishu, ni biashara inayokisiwa kuwa na thamani ya karibu dola nusu milioni kila siku.

‘Somalia kwa upande wake, inanufaika kwa biashara ya samaki wanaoingizwa Kenya’ anasema Ibrahim.

Uhamiaji:

Maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia wamehifadhiwa katika mojawapo ya kambi kubwa duniani ya Daadab iliopo nchini Kenya.

Kambi hiyo ya Dadaab ilijengwa mnamo 1991 kuzihifadhi familia za jamii zilizokuwa zinatoroka mzozo nchini Somalia, na baadhi ya watu wamekuwa wakiishi hapo kwa zaidi ya miaka 20.

Somalia inaitazama Kenya kama mshirika wake mkuu katika kufanya mageuzi ndani ya nchi hiyo.

Na huenda ndiyo mambo yanayostahili kupewa uzito kwa Rais Mohammed Abdullahi Farmajo na Rais Uhuru Kenyatta wanapotathmini na kutafuta suluhu kwa mvutano uliopo sasa, anasema mchambuzi Ibrahim.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents