Habari

Yaelezwa taifa la Nigeria kuwarudisha kwa ndege bure raia wake waishio Afrika Kusini

Yaelezwa taifa la Nigeria kuwarudisha kwa ndege bure raia wake waishio Afrika Kusini

Raia wa Nigeria wanaoishi Afrika Kusini wamepewa ofa ya ndege za bure kurejea nyumbani kukwepa vurugu za kibaguzi zinazoendelea Afrika Kusini. Wizara ya mambo ya Nje ya Nigeri imesema mmliliki wa Shirika la Ndege la Air Peace yupo tayari kuwasafirisha bure wale wote watakaotaka siku ya Ijumaa. “Wote watakaotaka huduma hiyo wanashauriwa kuwasiliana na Ubalozi wa Nigeria jijini Pretoria na ofisi ndogo za ubalozi jijini Johannesburg jwa matayarisho muhimu,” taarifa ya wizara imeeleza.

Mashambulizi ya biashara zinazomilikiwa na wageni nchini Afrika Kusini zimepokelewa kwa hasira kali na Wanaigeria ambao wanahisi wanalengwa na kuonewa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama amewaambia wanahabari siku ya Jumatano kuwa kulingana na taarifa zilizowafikia, hakuna raia wa Nigeria aliyepoteza uhai kwenye ghasia zinazoendelea. Hata hivyo, amesema kuwa serikali inaangalia uwezekao wa kumrejesha nyumbani balozi wake kutoka Afrika Kusini na kudai fidia kwa biashara zote za raia wa nchi hiyo zilizoshambuliwa. Nigeria imesusia kuhudhuria Mkutano wa Kimataifa wa Uchumi unaofanyika Afrika Kusini kutokana na ghasia zinazoendelea. Serikali ya Nigeria tayari imeshatoa onyo kwa rai wake waliopo Afrika Kusini wakiwataka kutosafiri ama kuelekea kwenye maeneo ambayo ghasia hizo zimeshamiri mpaka pale hali itakapotengemaa.

Waandamanaji NigeriaWaandamanaji nchini Nigeria wamevamia biashara za makampuni ya Afrika Kusini kulipiza kisasi, Mashambulizi ya kulipa kisasi kwa makampuni ya Afrika Kusini yaliyowekeza Nigeria pia yamefanyika, hali iliyoilazimu kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu- MTN – kufunga vituo vyake vya biashara kote nchini Nigeria. Mwanzoni mwa wiki Raisi Muhammadu Buhari alisema kuwa anamtuma mwakilishi wake kwenda Afrika Kusini kueleza ‘ghadhabu’ zao juu vurugu zinazoendelea.
Tiwa SavageMbali na hilo Mwandishi na muimbaji wa muziki nchini Nigeria Tiwa Savage amejiondoa kwenye tamasha alilokuwa amepanga kushiriki nchini Afrika Kusini baadaye mwezi huu kwa sababu ya ghasia zinazoendelea dhidi ya raia wa kigeni. Mwanamuziki huyo wa nyota wa mtindo wa Afrobeats salikuwa amepangiwa kufanya shoo katika jukwaa kuu la tamasha la DSTV Delicious Jumamosi ya tarehe 21 Septemba mjini Johannesburg, mji ambao kumeshuhudiwa ghasia kubwa na uporaji wa maduka mengi yanayomilikiwa na raia wa kigeni kutoka mataifa ya Afrika. Kablaya yake, msanii Burna Boy pia kutokanchini Nigeria ameapa kutokanyaga Afrika Kusini baada ya ghasia dhidi ya raia wa kigeni kuzuka upya nchini humo.
Burna BoyBurna Boy

Katika ujumbe kadhaa kwenye ukurasa wake wa Twitter masanii huyo mwenye miaka 28- alisema hajawahi kuzuru nchi hiyo tangu mwaka 2017 na hataki kurudi tena hadi serikali ya Afrika Kusini itakaposhughulikia suala hilo. Lakini serikali inatakiwa ”kufanya miujiza ila sijui jinsi itakavyoweza kutatau suala hili,” aliongeza.

Chanzo BBC.

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents