Tupo Nawe

Yafahamu mataifa haya 10 yaliyoongoza kwa kutekeleza hukumu ya kunyonga zaidi kuanzia mwaka 2013 hadi 2017

Yafahamu mataifa haya 10 yaliyoongoza kwa kutekeleza hukumu ya kunyonga zaidi kuanzia mwaka 2013 hadi 2017

Harakati za kupinga hukumu ya kifo duniani zimepamba moto. Kwa mujibu wa shirika la kmataifa la Kutetea Haki za Binaadamu la Amnesty International mpaka kufikia 2017 nchi 142 zimeacha kutoa hukumu ya kifo kisheria na/au kiutekelezaji. Umoja wa Mataifa (UN) unakadiria kuwa nchi 170 zimeachana na adhabu hiyo kwa nman moja au nyengine.

Kwa mujibu wa BBC. UN ina wanachama 193, hivyo ni mataifa 23 tu ndio ambayo inawezekana walitoa hata hukumu moja ya kifo katika muongo uliopita.

Kunyongwa

Mataifa ambayo yametekeleza hukumu ya kifo kati ya mwaka 2013 na 2017

Afghanistan, Bahrain, Bangladesh, Belarus, Botswana, Chad, China, Egypt, Equatorial Guinea, India, Indonesia, Iran, Iraq, Japan, Jordan, Kuwait, Malaysia, Nigeria, Korea Kaskazini, Oman, Pakistan, Palestina,

Saudi Arabia, Singapore, Somalia, Sudan Kusini, Sudan, Taiwan, Thailand, United Arab Emirates, Marekani, Vietnam na Yemen.

Nchi ambazo hazijatekeleza adhabu hiyo licha kuwepo kisheria kati ya 2013 na 2017

Tanzania si nchi pekee ambayo haitekelezi adhabu hiyo licha ya kuwepo kisheria.

Nchi nyengine zinazofanya hivyo ni pamoja na Antigua na Barbuda, Bahamas, Barbados, Belize, Comoros, Cuba, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Dominica, Ethiopia, Gambia, Guyana, Jamaica, Lebanon, Lesotho, Qatar, Saint Kitts na Nevis, Saint Lucia, Saint Vincent na Grenadines, Trinidad na Tobago, Uganda na Zimbabwe.

https://www.bbc.com/swahili/habari-48715412

By Ally Juma.

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW