Michezo

Yanga SC wapatwa na msiba mzito

Klabu ya Yanga imepatwa na msiba mzito wa baba yake mzazi na kocha mkuu wa klabu hiyo, Mzambia George Lwandamina.

Kocha wa Yanga, George Lwandamina

Taarifa hiyo  imethibitishwa na Afisa habari wa klabu hiyo Dismas Ten na kusema kuwa ni kweli kocha wao amepatwa na msiba wa baba yake mzazi huko kwao Zambia na tayari wameshafanya mpango wa kumsafirisha Lwandamina kwenda kuhudhuria msiba huo.

“Lwandamina ameondoka leo nchini Tanzania kuelekea nyumbani kwao Zambia kwa ajili ya mazishi ya baba yake, ila akifika huko ndiyo tutaweza kujua tarataibu za mazishi kwa kuwa shuguli zote zinafanyikia huko kwao”, amesema Ten.

Hata hivyo awali taarifa za kuondoka kwa kocha huyo nchini Tanzania zilieleza kuwa kuna matatizo ya kifamilia.

Bongo 5 Media inatoa pole kwa kocha Lwandamina na klabu ya Yanga kwa ujumla.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents