Habari

Young Dee aahadi laki 5 kwa mtu atakaesaidia kumpata mbaya wake

Vitendo vya watu kutumia majina ya watu maarufu kufungua akaunti katika mitandao ya kijamii na kuwatapeli watu imekuwa ikilalamikiwa na mastaa kibao hapa bongo. Awamu hii limemdondokea rapper Young Dee, ambaye sasa anamsaka kwa udi na uvumba mtu anaetapeli watu kwa jina lake.

young dee-2

Young Dee ameonesha kukerwa na tabia ya mtu ambaye amekuwa akitumia jina lake kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kutapeli watu ambao huwasiliana na mtu huyo wakijua ni yeye. Akiongea kupitia segment ya 255 ya XXL ya Clouds FM Young Dee amesema amekuwa akipata lawama kutoka kwa watu walioingizwa mjini na Yound Dee’ fake’ huyo ambaye inadaiwa anapoanza kuelewana na watu hao kwaajili ya show huaomba wamtumie kwanza elfu 50 kwa simu bila kuonana.

Kutokana na kukerwa na mtu huyo anayeendelea kumchafulia jina lake kwa watu, Young Dee ametangaza dau la shilingi laki 5 kwa yeyote anayeweza kumsaidia kumpata mtu huyo. “Mimi ntatoa laki 5 kwa mtu atakaesaidia kumpata huyo mtu”, alisema Young Dee

Haya deal ndo ishatangazwa na Young Dee, kama unahisi un auwezo na una moyo wa kumsaidia fanya hivyo laki 5 inakusubiri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents