Burudani

Young Killa atahadharisha uwepo wa account yake fake ya Facebook inayorubuni wasichana

Msanii mchanga wa muziki wa Bongoflava Young Killa amejikuta katika wakati mgumu baada ya mtu asiyemtambua kufungua account fake ya Facebook kwa kutumia jina la Young Kelleer Supernyota, kuwatapeli watu pesa na kuwarubuni wasichana.

DSC_0477

Killa ambaye ama hit na ngoma yake ya Dear Gambe, ameiambia Bongo5 kuwa mtu anayejiita Young Kelleer Supernyota katika facebook amekuwa akitumia jina hilo kuwarubuni wasichana na pia hivi karibuni kuingia makubaliano na mapromota na kuchukua pesa kama yeye ndie Young Killa halisi.

Young Killa amewaomba mashabiki wake wawe makini dhidi ya wahuni wanaotumia jina lake kutapeli na kufanya uhuni mitandaoni na kwamba akaunti yake halisi ni Youngkiller Msodoki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents