Burudani

Young Killer aitaja sababu iliyomfanya aanze ‘mapenzi’ mapema!

Enzi za mababu zetu vijana walianza mapenzi wakiwa na umri mkubwa na pengine baada ya kuoa au kuolewa kwanza.

11378657_377585389103775_1791900557_n

Maisha yamebadilika, vijana siku hizi wanajua mambo ya wakubwa wakiwa wadogo. Young Killer ni mmoja wa watu waliojanjaruka mapema.

“Ni kwasababu mimi nilikua tayari nipo active. Mimi nimeanza kujua vitu vingi mapema. Na hivyo vitu nilikuwa najifunza sababu mimi toka katika ukuaji wangu sijawahi kuwa na marafiki ambao nalingana nao,” Young Killer mwenye umri wa miaka 21 sasa alikiambia kipindi cha Chill na Sky.

“Kwahiyo unakuta kuna vitu nilikuwa nina uwezo wa kuiga.”

Rapper huyo mwenye uhusiano na msichana aitwaye Halimaty, amedai kuwa msichana huyo anaweza kuja kuwa mke wake.

“Naamini yule atakuja kuwa wife wangu kabisa na maisha mengine yataendelea sababu nampenda sana na yeye ananipenda vile vile.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents