Michezo

Zanzibar Heroes yafuta machungu ya Watanzania, Ndoto ya Wakenya yatimia CECAFA

Timu ya taifa ya mpira wa Miguu visiwani Zanzibar, Zanzibar Heroes imewatoa kimasomaso Watanzania baada ya ushindi wa goli 2-1 dhidi ya timu ya bora zaidi ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Timu ya taifa ya Uganda na kufanikiwa kutinga fainali ya michuano ya CECAFA.

Zanzibar Heroes

Kwa ushindi huo Zanzibar inakuwa timu ya pili kutopoteza hata mchezo mmoja kwenye michuano hiyo ikifuatiwa na wenyeji timu ya taifa ya Kenya.

Ushindi huo kwa upande mwingine unakuwa umefuta maumivu kwa Watanzania kwani timu ya Tanzania bara, Kilimanjaro Stars imeshatupwa nje ya michuano hiyo mapema kitu ambacho kimeleta gumzo kwa wadau wa soka nchini wengi wakidai kikosi hicho kifumulie na kuundwa upya.

Zanzibar Heroes sio tu wamewafurahisha Watanzania bali pia wamewafurahisha Wakenya kwani jana Desemba 14,2017, baada ya timu yao ya taifa kufuzu walisikika wakikiri wazi kuwa timu wanayoihofia kwenye michuano hiyo ni Uganda huku wakisema kuwa maombi yao yote yapo Kwa Zanzibar Heroes ishinde dhidi ya Uganda ili waweze kujiweka sehemu nzuri ya kushinda Kombe hilo.

Tunafurahi timu yetu kufuzu tunajua michuano ni migumu ila fainali yetu itakuwa nzuri kama kesho (leo) Uganda itafungwa ili tukutane na Zanzibar kwani Uganda wapo vizuri na timu yao ni bora zaidi yetu“amesema Shabiki mmoja kupitia KBC aliyejitambulisha kwa jina la Otieno jana baada ya Kenya kushinda mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Burundi.

Fainali ya michuano hiyo itachezwa jumapili ya Desemba 17, 2017 majira ya saa 9:00 alasiri ambapo Kenya itawakaribisha Zanzibar Heroes, huku mchezo wa mshindi wa tatu wa michuano hiyo kati ya Uganda na Burundi utachezwa saa 7:30.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents