Burudani
Zari the Bosslady ni mwendo wa helikopta tu Kenya (Picha)
Wakati ambapo Diamond Platnumz aliitumia siku yake ya Jumapili kuonesha baadhi ya utajiri wake, baby wake Zari the Bosslady alikuwa jijini Nairobi akiishi makubwa!
Zari akiwa kwenye helikopta pamoja na Juliana Kanyomozi?
Weekend hii Mrs Chibu alikuwa Nairobi ambapo aliungana na bosslady mwenzake, Huddah Monroe kwenye party ya Art of Luxury iliyofanyika Skylux Lounge.
Baada ya party hiyo, Zari alikodi chopper kuzunguka katika maeneo kadhaa ya Kenya ikiwemo Naivasha.