Habari

Zeb Matabane hajaondolewa kwenye tamthilia ya Isidingo, Endemol wasema

Kampuni ya Endemol imekanusha tetesi kuwa muigizaji, Don Mlangeni anayejulikana kama Zeb Matabane kwenye tamthilia maarufu ya Isidingo ya Afrika Kusini kuwa amefukuzwa.

Zeb

Gazeti la Daily Sun liliripoti kuwa Mlangeni, aliondolewa kwenye show hiyo baada ya kudaiwa kukataa kuipa shavu benki kubwa iliyokuwa imetajwa kwenye script.

“Ilikuwa sehemu ya script na alipotakiwa kulitaja jina hilo aliruka. Mabosi hawakufurahi,” kilisema chanzo kilicho karibu na show hiyo.

Vyanzo vingine vilisema kuwa Mlangeni alihisi alikuwa akitumiwa na kulipwa fedha kidogo. Alidai kuwa yeye aliendelea kupata mshahara wake wa mwezi bila bonus ama pesa za ziada kwa kuitangaza

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents