Michezo

Zifahamu timu tano zilizofanikiwa kushinda taji la NBA mara nyingi zaidi

Moja ya mashindano yanayofuatilia kwa ukaribu na watu wengi zaidi duniani moja apo ni ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani NBA ambayo pia inashirikisha timu moja kutoka Canada ambayo ni Toronto Rapters ikiwa Marekani pekee ina timu 19.

Usiku wa kuamkia leo timu ya Los Angeles Lakers wamefanikiwa kuibuka kuwa mabingwa wapya wa ligi hiyo kwa ushindi wa pointi 106-93 dhidi ya wapinzani wao Miami Heat.

Ushindi huo umeifanya LA Lakers kuibuka na ushindi wa jumla ya michezo 4-2 dhidi ya Miami Heat ambapo ilitegemewa na wengi kwenda mpaka game 7 kutokana na upinzani mkubwa ulioonyeshwa na Miami Heart.

Kwa upande wa Lakers Huu unakuwa ubingwa wao wa 17 kwa kufanikiwa kuikiifikia timu nyingine kutoka NBA ambayo ilifanikiwa kushinda mara nyingi ambayo ni Boston Celtics ambao waliongoza kwa kipindi kirefu sana.

Katika ushindi huo, Nyota wa Los Angeles Lakers Lebron James alichangia kwa kiasi kikubwa katika ushindi huo kwa kufunga triple double pointi 29, rebound 14, na assists 10.

Lebron James alimaarufu King James Ameshinda tuzo ya Mchezaji bora mwenye thamani zaidi (MVP) katika Fainali za NBA.

Nyota huyo wa timu ya Los Angeles Lakers sasa ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya NNE:

🏆 2012 ✅
🏆 2013 ✅
🏆 2016 ✅
🏆 2020 ✅

Licha ya ubingwa huo wa Lakers zifahamu timu tano zilizofanikiwa kushinda taji hili mara nyingi zaidi katika historia ya NBA Marekani.

1  Boston Celtics- 17
2. LA LAKERS- 17 🆕
3. Chicago Bulls- 6
4. Golden State Warriors- 6
5. San Antonio Spurs- 5

Huku mabingwa wa ligi hiyo msimu uliopita Toronto Rapters ambao walishinda kwa msaada mkubwa wa nyota wa Los Angeles Clipers Kawl Leonard wakiwa wameshinda mara moja tu ingawa kwa upande wa Division titles wakiwa wameshind amara 7.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents