Burudani

ZIFF kuonesha filamu ya Winnie Mandela

Zaidi ya wadau 50 wa filamu duniani wanatarajiwa kuungana pamoja Julai 8 hadi 16 mwaka huu katika Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe, visiwani Zanzibar.

Tamasha hilo la 20 linatarajiwa kuonesha filamu zaidi ya 100 kati ya filamu hizo, ipo filamu ya mwanaharakati Winnie Mandela kutoka Afrika Kusini iliyoongozwa na Pascale Lamche, na nyingine ni ya Whitney Houston ya ‘Can I Be Me’ iliyotengenezwa na Nick Broomfield, pamoja na makala ya mtayarishaji na mwigizaji maarufu kutoka Hollywood, Leonardo di Caprio inayoitwa ‘The Ivory Game’.

Watengeneza na  wataarishaji filamu kutoka nchi zaidi ya 70, wametuma filamu zao kwa ajili ya tamasha hilo. Tanzania ni moja wapo ,Kenya, Canada, Hispania, Ufaransa, Afrika Kusini, , India, Australia, Marekani, Nigeria, Rwanda, Brazil, Ghana, Chad, Uganda, Msumbiji, Hungary, Uingereza na Ethiopia pia.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents