Habari

Zimbabwe hali si shwari, Jeshi lazingira kituo cha utangazaji cha taifa

Jeshi la Zimbabwe limezingira kituo cha utangazaji cha taifa nchini humo, (ZBC) likidai kuwa linachukua hatua ya kuwalenga wahalifu na kurudisha amani nchini humo.

Jeshi hilo linasema kuwa hayo sio mapinduzi ya kijeshi dhidi ya Rais Mugabe kama wengi wanavyodhani kwani Rais Mugabe bado yupo madarakani na yuko salama.

Baada ya tukio hilo la wanajeshi kuzingira na kudhibiti kituo hicho cha habari, imeripotiwa kuwa asubuhi ya kuamkia leo milio ya risasi ilisikika katika maeneo ya kaskazini mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Harare.

Kwa mujibu wa maelezo kutoka katika gazeti la News 24 linadai kuwa moja ya viongozi wa jeshi hilo ambaye hakutaka kujitambulisha amesema  jeshi hilo linataka kukabiliana na watu ambao wanatenda uhalifu unaoleta madhara ya kijamii na kiuchumi nchini Zimbabwe.

Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotolewa na Rais Mugabe na hakuna mfanyakazi wa Shirika hilo la utangazaji aliyejeruhiwa kwenye ufamizi huo wa majeshi.

Hali ya usalama nchini Zimbabwe imekuwa tete tangu Rais Mugabe amtoe madarakani aliyekuwa makamu wake wa Rais, Emmerson Mnangagwa.

SOMA ZAIDI-Rais Mugabe amtumbua Makamu wake wa Rais

Tayari ofisi zote za kiserikali nchini humo zimefungwa ikiwemo ubalozi wa Marekani nchini humo ambao kupitia ukurasa wao wa Twitter umetangaza kuwa leo hautafungua ofisi zake mpaka hali itakapotengamaa.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents