Zitto Kabwe aiiomba serikali iyabane makampuni ya simu yawalipe zaidi wasanii kwa ringtones



Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mheshimiwa Zitto Kabwe amemuomba naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na technolojia Mhe. January Makamba kuhakikisha kuwa anawasaidia wasanii kulipwa zaidi na makampuni ya simu kutokana na kutumia nyimbo zao kama miito ya simu, ring tones na ring back tones.
“Artists earning only 7% of the revenue generated by their own songs? Network providers pocketing 80%? NO. Kaka @JMakamba stand against this,” Mhe. Zitto ametweet asubuhi ya leo.
Mheshimiwa Zitto amenukuu takwimu zilizoandikwa kwenye makala ya gazeti la The Citizen iliyopewa kichwa cha habari kisemacho: How Bongo artistes miss billions in ringtoine deals. “Ringtone/Callertone sub-sub-sub-sector is a tshs 40bn industry. A major stakeholder, ARTIST, gets 7%! Networks whopping 80%, middlemen 13%!”
“The state is obliged to protect the weak against the giants. That’s why markets are regulated. Telecom MUST give our artists fair share, aliandika.”
“Makamba simamia maslahi ya wasanii wetu. Hili lako na kwa pamoja twaweza. Kampuni za simu zapata mabilioni, wasanii? Samahani nimekuamkia asubuhi maana najua unafuatilia jambo hili na kesho ni Wizara yenu. Usikubali maelezo ya kirasimu. Vijana tu, aliendelea kusisitiza.
“Hawa vijana @MwanaFA @linex_tz @ChegeChigunda @mwasitiJ @diamondplatnumz @ommydimpoz @AyTanzania wanahangaika, wanapigana, wanapata 7%… NO.”
“Hawa vijana wasanii wanapaswa kuwa mabilionea na walipa kodi wakubwa sana. Lazima tuwatetee.”
Mheshimiwa Zitto ameongeza kuwa pamoja na kwamba vyombo vya habari pia vinapaswa kuwalipa wasanii kwa matumizi ya kazi zao, bado haviwezi kuwaingizia pesa kama makampuni ya simu yakiwalipa kile wanachostahili.
“Hakuna pesa huko. Huku kwenye simu ndio kuna pesa. Tunaanzia huku ili wasanii wawe na nguvu ya kupambana na radios. Tunaanza na Wizara ya Habari, kisha Mawasiliano na baadaye wizara ya Biashara. Lazima wasanii kupata stahiki yao kwenye ringtone business.”
Inadaiwa kuwa makampuni ya simu huingiza zaidi ya shilingi milioni 80 kila moja kwa siku kutokana na matumizi ya nyimbo za wasanii kwaajili ya ringtones na kwa mwaka makampuni hayo kwa pamoja huiingiza zaidi dola bilioni moja zinazotokana na huduma yanayozitoa.
Mheshimiwa Zitto amekuwa karibu zaidi na wasanii siku za hivi karibuni na amesaidia kuanzishwa kwa kundi la Kigoma All Stars linalotamba sasa na wimbo wake ‘Leka Dutigite’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents