Habari

98 Degrees kurejea tena baada ya miaka 11


Kundi maarufu la 98 Degrees linatarajiwa kujiunga tena kwaajili ya kufanya kazi pamoja tangu kuwa kimya kwa miaka 11.
Fununu za kurejea kwa kundi hilo kwenye muziki zilianza kusambaa mwezi March mwaka huu baada ya website yao rasmi kuwa updated ghafla.
Ingawa kiongozi wa kundi hilo Nick Lachey alikanusha, alitweet kwa kuandika “#neversaynever”.
Jana Nick amemuambia mtangazaji, Ryan Seacrest, “Nadhani wote tumekuwa na bahati tangu tuperform mara ya mwisho miaka 11 iliyopita kwa kuendelea kufanya mambo binafsi.”
Nick aliendelea, “Tunamiss raha ya kuwa kwenye stage, kutumbuiza pamoja, na pia mashabiki wamekuwa wakituomba sana, kwahiyo inaonekana ni sawa tukirudi. Mara zote tumekuwa tukisema kuwa kundi halijavunjika, tulikuwa tunapumzika tu na sasa inaonesha ni muda muafaka wa kuweka kila kitu pamoja tena.”
Mwezi August mwaka huu wataonekana kwa mara ya kwanza kwenye tamasha la MixTape (Festival) huko Hershey, Pennsylvania ambapo pia makundi ya The Wanted, New Kids On The Block na Backstreet Boys yatatumbuiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents