WAREMBO MISS DAR INTERCOLLEGE WAFUNDWA


KAMATI ya Miss TAnzania jana imetembelea kambi ya Miss Dar Intercollege
iliyopo kwenye hoteli ya The Grand Villa, Kijitonyama jijini Dar es Salaam
kwa lengo la kuwafunda.
Shindano hilo linatarajiwa kufanyika ijumaa ya kesho katika ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa uliopo mkabala na chuo cha Usmiamizi wa Fedha (IFM).
Akizungumza na warembo hao, mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania
Albert Makoye aliwataka warembo hao kufuata miongozi na kanuni za shindano
hilo ikiwemo kuwa na nidhamu.
Alisema urembo si sura na umbo zuri bali unahusisha pia nidhamu katika jamii
hivyo amewataka warembo hao kuzingatia hayo.
“Nafahamu ninyi ni wasomi wazuri hivyo mmeyapokea vema mafunzo
tuliyowapa…hatutarajii kusikia mmoja wenu anachafua hali ya hewa katika
siku za usoni na mambo ya skendo skendo,”Alisema Makoye.
Dina alisema shindano hilo litapambwa na msanii wa uziki wa kizazi kipya
nchini Nasib Addul ŒDiamond¹ sambamba na bendi ya Skylight iliyopo chini ya
mshiriki wa Tusker Project Fame mwaka juzi, Anneth Kushaba. ³Mwaka huu
tumejipanga vema kuhakikisha mmoja ya warembo kutoka Miss Dar Intercollege
anafanya vema katika fainali za Miss Tanzania ,²alisema Dina. Warembo
watakaoshiriki shindano hilo wanatoka vyuo vya Biashara (CBE), Uandishi wa
Habari (DSJ) na Time, Ustawi wa Jamii, Usimamizi wa Fedha (IFM) na Chuo
Kikuu huria (OUT ambapo taji linashikiliwa na Rose Msuya kutoka IFM, huku
mshindi wa pili wa mwaka jana, Blessing Ngowi alitinga fainali za Miss
Tanzania. Dina aliwataja warembo hao kuwa ni pamoja na Veronica Ngota, Rose
Muchunguzi, Nancy Maganga, Hilda Edward, Diana Nyakisinda, Neema Michael,
Veronica Yollla, Jacquiline Cliff, Sharifa Ibrahim, Natasha Deo, Saada
Suleiman, Rose Masanja na Jamila Hassan. Shindano hilo limedhaminiwa na
kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Redd¹s,Dodoma Wine, Ndege
Insurance, Skylight Band,Lamada Hotel, Screen Masters,Makumbusho ya Taifa,
Mustafa Hassanali, Shear Illusions, Lamada Hotel,Grand Villa Hotel, Sporti
Kizaa zaa, Clouds Fm na blog za Michuzi, dina ismail (zamani Mamapipiro),
Bin Zubeiry,Mtaa kwa Mtaa na Fullshangwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents