Michezo
Yanga wamtimua kocha Marcio Maximo
Klabu Yanga imevunja mkataba na kocha wake, Marcio Maximo usiku wa kuamkia leo.
Sababu za kutimuliwa kwa kocha huyo kutoka Brazil ni ufanisi mbovu wa timu ya Yanga iliyochapwa 2-0 na Simba katika mtanange wa Nani Mtani Jembe mwishoni mwa wiki.
Sasa nafasi ya Maximo itachukuliwa na Van Der Pluijm kutoka Uholanzi. Aliwahi kuifundisha Yanga kwa nusu msimu baada ya kufukuzwa kwa Ernst Brandts ambaye pia alitoka Uholanzi.