Hawa ni wachezaji walioondoka Manchester United masaa machache kabla ya kufungwa kwa usajili
Huku dirisha la usajili barani Ulaya likiwa limebakisha masaa machache kufungwa, klabu ya Manchester United imeendelea kupunguza kikosi chake ikiwa ni pamoja na kuwaondoa kikosini wachezaji wasio na nafasi.
Javier Hernandez karuhusiwa kuondoka na sasa amesajiliwa na Bayern Leverkusen ya Ujerumani kwa pound £12m.
Mchezaji mwingine ni Adnan Januzaj ambaye amejiunga na Borusia Dortmund ya Ujerumani kwa mkopo wa msimu mzima.
Beki John Evans ameuzwa kwa pound milioni 6 na amejiunga na klabu ya Westbromwich Albion.
Na golikipa wa Manchester United, Anders Lindegaard amejiunga na West Brom kwa mkataba wa miaka miwili.
Golikipa namba moja wa Manchester United, David De Gea usajili wake kwenda Real Madrid bado umekwama baada ya jana usiku dirisha la usajili nchini Hispania kufungwa huku golikipa huyo akiwa tayari yupo nchini kwao akisubiri dili likamilike ili aweze kujiunga Madrid.
Na sasa unasubiriwa utaratibu mwingine utakapofanyika ikiwa ni pamoja na kuomba ruhusa ya FIFA.