Burudani
Bobby Shmurda aenda miaka saba jela
Baada ya kukubaliana na upande wa mashtaka, rapper Bobby Shmurda kutoka Brooklyn, amehukumiwa kwenda jela miaka saba Jumatano hii.
Mwezi uliopita, Bobby alikiri mashtaka ambayo yaliyokuwa yanamkabili ya kumiliki silaha kinyume cha sheria. Shmurda aliambia mahakama kuwa alilazimishwa na mwanasheria wake kukubali hukumu hii ili asihukumiwe miaka mingi zaidi.
Mwanzo alikuwa amehukumiwa miaka 5 lakini alikuwa hajakubali kwasababu rafiki yake, Chad “Rowdy Rebel” Marshall alikuwa amehukumiwa miaka 12 kwahiyo ikabidi aongezewe ili rafiki yake apunguziwe. Wote wamehukumiwa miaka 7 na mahakama.