Hasira zapelekea Miss KK kuchora tattoo za kutosha
Msanii wa muziki Bongo, Miss KK ametoa sababu ya mwili wake kuwa na tattoo nyingi.
Akizungumza na Bongo5 Miss KK amesema tattoo zake zilisababishwa na hasira baada ya mama yake mzazi kumfukuza nyumbani na kupata ujauzito akiwa katika umri mdogo.
“Tattoo zangu zimetokana nilikuwa na hasira from myself, nilikuwa najilaumu for many things kwanini nimepata mimba for very young age, kwanini mama yangu alinifukuza, so I was very confused child, nilikuwa nimechanganyikiwa kinamna tuseme” amesema.
“So nikaamua the way to take out my pain ni kuchora tattoo, wakati huo nina mimba ya mtoto wangu wa kiume, so niliweka tattoo tatu kwa wakati mmoja because hizo tattoo have been mean behind, niliweka tattoo ya mtoto wangu na jina lake kabla hajazaliwa” amemaliza kwa kusema Miss KK.