Fahamu
Kutana na Cresencio na Howard X marafiki wanaofanana na Rais Duterte na Kim Jong Un (+picha)
Wahenga waliosema dunia wawili wawili, ama hakika hawakukosea kwani sio kwa maswahiba hawa wawili, Cresencio Extreme na mwenzake Howard X ambao wote wanafanana sawia na marais wa Ufilipino na Korea Kaskazini.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, umeeleza kuwa wawili hao walikuwa pamoja katika barabara za mji wa Hong Kong, wakipiga picha wikiendi iliyopita na kula pamoja chakula cha jioni katika mgahawa mmoja jijini humo.
Cresencio Extreme amefanana na Duterte na huku mwenzie Howard X anayefanana na Kim Jong un.
Picha na Reuters