Michezo
Wachezaji, kocha wa kigeni vibali vya kazi vyatakiwa kuwasilishwa Uhamiaji
Klabu zote nchini ambazo zimeajiri wachezaji na makocha wa kigeni zimetakiwa kuwasilisha orodha ya Waajiri hao pamoja na vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini katika Idara ya Uhamiaji klaba ya kuanza mashindano ya msimu huu.
Hivyo, klabu za Mkoa wa Dar Es Salaam zinatakiwa kuwasilisha taarifa hizo ofisi ndogo ya Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji iliyoko Kurasini, wakati nyingine ziwasilishe ofisi za Uhamiaji za mikoa yao.