Gaitano Kagwa kusherehesha shindano la Miss East Africa 2012
Mashindano ya Miss East Africa 2012 yanafanyika leo katika ukumbi wa Mlimani City Dar es salaam.
Kwa mujibu wa taarifa ya mtayarishaji wa mashindano hayo Rena Callist amesema washiriki watakaopanda kuchuana tayari wamejiandaa vema.
Mshehereshaji wa onesho hilo ni mtangazaji wa kituo cha m-net Gaetano Kagwa aliyewahi kuiwakilisha Uganda kwenye shindano la Big Brother Africa.
Jumla ya zawadi zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 100 zitatolewa kwa washindi wa mashindano hayo.
Washiriki katika pambano hilo ni kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda,Burundi, Somalia, Djibout,Sudan, Eritrea, Sudan Kusini na Shelisheli.